Monday, February 16, 2009

TUMEFANYA KAZI KUBWA na Pact Tanzania pale Nzega na Igunga


ASALAAM ALEIKUM NDUGU !
Mwaka 2007/2008/2009 ni mwaka tuliofanya kazi kubwa za kihistoria za kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pale Igunga na Nzega. Mimi (John Mbele) nikiwa nafanya kazi katika shirika lisilokuwa la kiserikali la JIDA, tukifadhiliwa na Pact Tanzania. tumeweza kusaidia watoto 3,511. tumeweza kuwapatia unifomu za shule, vifaa vya shule, ada, bima za afya, mbuzi ( kwaajili ya kuimarisha hali zao za kiuchumi), huduma za kisaikolojia nk.

unaweza kuona baadhi ya picha za watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.Wafanyakazi wa pact wamekuwa karibu sana kuhakikisha kuwa kazi hizo zinafanyika vizuri, wanatoa ushauri mara kwa mara na kutembelea baadhi ya walengwa ili kubadlishana nao mawili matatu. Deo Seimu ametembelea mara ya mwisho, mwezi Januari mwaka huu 2009 na kushiriki baadhi ya shughuli zinazoendelea.

Naandaa makala kuuuubwa na nitaiweka katika blog hii na blog ya JIDA, nitasema mambo kibao, nitawawekea picha kibao, zingine zinatia moyo, na kama kawaida zingine zinatia huruma kidogo, hasa pale utakapoona maisha ya watoto wetu: wanavyohangaika na bila kuwa na mwelekeo.

JAMANI, KILA MTU ASAIDIE WATOTO WETU PALE ANAPOWEZA, KWA KADIRI YA UWEZO WAKE. LINAWEZEKANA KAMA KILA MMOJA WETU ATATIMIZA WAJIBU WAKE.

Mbele, John.

1 comment: